published on in Quick Update

Jinsi vita vya Israel huko Gaza vinavyotegemea nguvu ya Yahya Al-Sinwar - Jerusalem Post

15 Februari 2024

Magazeti ya kimataifa, Israel na Kiarabu yaligusia vita vya Gaza, yakizungumzia operesheni ya kijeshi ya ardhini ambayo jeshi la Israel huenda likafanya huko Rafah, kusini mwa Ukanda wa Gaza.

Magazeti yaliwasilisha njia za kumaliza vita, mengine yameonya kuhusu matokeo mabaya ikiwa uvamizi wa ardhini utafanywa, huku baadhi ya magazeti yakiwasilisha maoni kuhusu mustakabali wa Gaza na kipindi cha baada ya vita.

Tunaanza ziara yetu na gazeti la Israel "Jerusalem Post", ambalo lilikuwa na kichwa cha habari "Vita vya Israel huko Gaza vinategemea kabisa maoni ya Yahya Sinwar." Mwandishi wa Israel Mika Halpern anazungumzia nafasi ya mkuu wa ofisi ya kisiasa ya Hamas katika Ukanda wa Gaza, katika vita vinavyoendelea hivi sasa.

Habern anaeleza kuwa Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu anakabiliwa na shinikizo kubwa ndani ya Israel, pamoja na shinikizo la kimataifa kutoka kwa madola ya kikanda.

Lakini inaashiria shinikizo kubwa zaidi lililotolewa na Ikulu ya Marekani, kama alivyoiweka.

Mwandishi wa makala hayo anaamini kwamba Rais wa Marekani, Joe Biden, si tu kwamba anamshinikiza Waziri Mkuu wa Israel kwa sababu za kijeshi, bali anaamini kwamba vita vya Israel dhidi ya Hamas huko Gaza vinaweza kuhatarisha nafasi yake ya kuchaguliwa (tena) mwezi ujao wa Novemba, na kwa sababu hii Ikulu ya White House inataka Israel isimamishe vita sasa."

Mwandishi anaendelea katika makala yake kwa kusema kwamba vita vitakwisha bila shaka, si kwa sababu ya shinikizo ambalo Netanyahu anapatiwa, bali kwa sababu ni lazima kumuondoa Yahya Sinwar.

Mwandishi wa Israeli anaelezea Sinwar kama "mhimili" wa vita vya sasa.

Mwandishi anasema kwamba hajali kuhusu hatima ya Sinwar, kama aliuawa, alikamatwa, alijiua, alikimbilia Misri na kisha kwingineko, au kama alikuwa sehemu ya mpango wa mateka uliomruhusu kwenda uhamishoni.

Jambo muhimu zaidi kwake ni kwamba "Sinwar hapaswi kuwepo tena au kuleta tishio," na kwamba hapaswi kuwa na uwezo wa kutoa changamoto kwa Israel na kuwahamasisha Hamas, hata kutoka mbali.

Micah Halpern anaamini kwamba Sinwar ndiye "mtu anayeamua hatima ya vita vya Israel na Hamas," kwani kunusurika kwake kunawapa wapiganaji wa Hamas msukumo wa kuendelea na mapambano yao, na "kama kiongozi wao anaweza kunusurika, wataweza pia kunusurika."

Mwandishi wa makala ya Israel anaeleza kuwa kumpata Sinwar "haimaanishi kukatwa tu kichwa cha nyoka wa Hamas," kwani hakuna mtu mwingine ndani ya Ukanda wa Gaza anayeweza kuchukua nafasi yake.

Wale wanaoishi nje ya Ukanda wa Gaza hawana uaminifu, kwa sababu hawana uzito unaohitajika kuwahamasisha Hamas kuendeleza vita vyake.

Lakini kuendelea kuishi kwa Sinwar ndiko kunachukuliwa kuwa chanzo cha msukumo kwa wapiganaji wa Hamas, kama mwandishi anavyosema.

Kwa nini Marekani haizuii shambulio la ardhini huko Rafah?

Tunaendelea na makala nyingine ya maoni yenye kichwa “Marekani inaweza kukomesha ukatili unaofanywa leo huko Rafah. Kwa nini isiwe hivyo?” Ni katika gazeti la Uingereza The Guardian, na Paul Rogers, profesa wa heshima wa masomo ya amani katika Chuo Kikuu cha Bridford.

Mwandishi huyo wa Uingereza anaonya kwamba shambulio lolote la ardhini la Israel dhidi ya mji wa Rafah litakuwa na hatari, na litaathiri moja kwa moja jiji hilo na mazingira yake, ambayo ni makazi ya “watu wapatao milioni 1.5, wengi wao wakiwa kwenye mahema hafifu, wakikabiliwa uhaba wa chakula na maji safi, pamoja na ukosefu wa msaada wa matibabu.”

Paul Rogers anaamini kwamba Marekani inaweza kukomesha uvamizi wa ardhi ya Rafah, kwani "Israel inategemea sana msaada wa kijeshi wa Marekani na haiwezi kuendeleza vita kwa muda mrefu bila hiyo."

Rogers pia anasema kuwa utawala wa Biden umetuma ujumbe mkali kwa Netanyahu ili kupunguza vifo vya raia wa Palestina, lakini haujafanikiwa sana.

Mwandishi wa makala anaelezea kutofaulu kwa ujumbe huu kwa kusema kwamba "Waisraeli wanajua kwamba wanaweza kupuuza Biden bila matokeo."

Kulingana na mwandishi wa Uingereza, hakutakuwa na matokeo ya kumpuuza Biden "kwa sababu ni hakika kwamba kushawishi kwa Israel kuna nguvu sana huko Washington, na kwamba uhusiano wa Pentagon (Idara ya Ulinzi ya Marekani) na Israeli ni ya kina."

Mwandishi anaendelea kueleza kwamba uhusiano huu mkubwa kati ya Pentagon na Israeli uliimarishwa sana wakati ushauri wa Israeli ulipoombwa wakati wa Vita vya Iraq mwaka 2003, na mpaka sasa majeshi ya Marekani yamewekwa kwa kudumu nchini Israel na yanaendesha kituo kikubwa cha tahadhari cha rada.

Mwandishi anaamini kwamba kuna sababu nyingine ya kupanua ushawishi wa Israel ndani ya Marekani, ambayo ni uwepo wa kundi kuu la shinikizo la Israel, au "American Israel Public Affairs Committee" inayojulikana kwa ufupi kama "AIPAC", ambayo ina jukumu madhubuti. .

Hatahivyo, pia kuna mashirika ya Kiyahudi ya Marekani huko Washington ambayo hayajaridhika na vita, kama vile kikundi cha J Street, kwa mujibu wa mwandishi.

Mwandishi wa makala hiyo anaongeza kuwa kuna sehemu inayokosekana ya msimamo wa Biden, ambayo ni faida ambayo Israel inapata kutokana na kuungwa mkono na Wakristo ndani ya Marekani.

Miongoni mwa Wakristo wa evanjeli wapatao milioni 100 katika Marekani, “kuna watu wachache sana wanaoshikilia imani kwamba Israeli ni sehemu muhimu ya mpango wa Mungu, kwa ajili ya siku ya mwisho,” kulingana na maneno ya mwandishi Mwingereza Paul Rogers.

Wengi wao pia wanaamini, kulingana na kile ambacho mwandishi anasema, “kwamba vita vya mwisho vitakuwa katika Nchi ya Israel kati ya wema na uovu, na kwamba hii ni sehemu ya mpango wa Mungu kwa Israel kuwa taifa la Kiyahudi.”

Mwandishi wa Uingereza Paul Rogers anahitimisha makala yake, akinukuu kauli za Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron na mratibu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya, Josep Borrell, waliposema kuwa Marekani lazima iangalie upya msaada wa kijeshi kwa Israel.

Mwandishi anaongeza, "Juhudi zaidi zinahitajika haraka ikiwa tunataka kuzuia janga kubwa."

Imetafsiriwa na Lizzy Masinga

ncG1vNJzZmivp6x7o67CZ5qopV%2BoxKK0yKWgaJmiqbakuMSsZpxom5m3uYXXqWywpw%3D%3D